Welcome
Thursday, May 30, 2013
Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka!
Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana
imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la
Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu,
Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo
yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na
57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita
ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha
kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka
asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia
asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao
awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na
kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri
kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya
349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment