Welcome
Tuesday, June 18, 2013
Wednesday, June 5, 2013
Sunday, June 2, 2013
PICHA: ndani ya BAGAMOYO dip one wote wakisheherekea ushindi wa USTAWI football & netball league interclasses....!!!
tunawasikiliza viongozi ongeeni tunaelekea wap
wenye michina hatukua nyuma kupiga picha pia
I LOV THIIIIIIIIIIISSS
mjengoo hatari ndan ya Bwaga moyo
Saturday, June 1, 2013
washindi ustawi Interclasses
Timu ya mpira wa miguu kutoka diploma 1 wamechukua ubingwa upande wa mpira wa miguu katika mashindano ya madarasa Institute of Social Work ambapo walicheza finali na diploma 2 human resource. Katika mchezo huo uliomalizika kipindi cha pili kwa timu hizo kufungana goli 2-2 na kuingia katika matuta ambapo dioloma 1 walitangawa mabingwa. nayo timu ya wasichana ya diploma 2 human resource imeshinda mchezo wao fainali dhidi ya diploma 1na kuibuka washindi upande wa netboli.
mpira ukiendelea
mtanange ukiendelea
Waziri akienda kumalizia penalti ya mwisho
washindi wakiwa wameshikilia chaoo..tarehe 31 usiku baada ya ushindi
kipa Michael mkamba(kulia) na captain Hero Lusanga (kushoto) wa timu ya diploma one
source social work blogsite
Friday, May 31, 2013
weraaa weeeeeraa hizi ndizo Picha za mashabiki wakiisuport timu yao
wakiwa makini kuangalia mpira ulokua unaendelea huku zikiendelea shamra shamra kwa mavuvuzera
CR wa dip one akimpa ushauri kocha wa dip one kuhusu mchezo katika mechi hiyo
coach bwana Anuary Mgalu na mchezaji wake Msaada peter wakishangilia baada ya mechi
weeeeeeeeeeeeeeeeeeerrrrrrrrrrrrrraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
mpaka kielewekeeee mpaka majogoooo
Hatimaye DIPLOMA one wachukua ushindi katika fainali ya ligi ya interclasses 2012/2013
kikosi cha diploma one wakijiandaa kuanza mechi hyo..kushoto->kulia ni Adam,sheami,peter,hussen,hafidhi na Hero
ni mshambuliaji Hero akisalimiana na wachezaji wa timu pinzani tayari kuanza mechi Dip VS bach 2..walfungana kwa penalt 5-4.
ni kipa machachali bwana michael mkamba akijiandaa vizuri kuenda kuanza kupangua mikwaju ya penalt

Thursday, May 30, 2013
Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka!
Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana
imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la
Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu,
Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo
yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na
57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita
ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha
kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka
asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia
asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao
awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na
kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri
kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya
349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
The HEROES-Diploma one 2012/2013 ISW
Friday, May 24, 2013
Kesi ya Mabomu-Arusha
Polisi wamewaachia wote waliokamatwa kuhusika na kulipuwa waumini wa kanisa katoliki Arusha na kubakiwa na mmoja Victor Ambrose ambaye sasa anatuhumiwa na kushtakiwa kwa kupanga njama, kupata bomu, kurusha bomu na kuuwa na kujeruhi. Kijana mwenye miaka 20 ambaye elimu yake darasa la saba, mwendesha bodaboda ameweza kujipatia bomu la kutengenezwa kiwandani, kujua kulitumia bila mafunzo, kulirusha na kuuwa. Je alikuwa ana motives gani? Kwanini? Alinunua au alipata bomu wapi? Nani alimletea Arusha au alilipata Arusha?
Je Victor alikwenda na nani kanisani? nani alikuwa abiria na yuko wapi? Kwanini polisi hawataki kugusia kuhusu abiria wa Victor?
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewaachia kwa dhamana watuhumiwa wanaodaiwa kurusha bomu kwa waumini waliokuwa wamekusanyika kuanza ibada ya uzinduzi wa Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti, Mei 5, mwaka huu, jijini Arusha.
Hata hivyo, watuhumiwa hao wamepewa sharti la kuripoti polisi, pindi watakapohitajika kufanya hivyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema wamelazimika kuwaachia kwa dhamana kwa kuwa sheria haiwaruhusu kuendelea kuwaweka mahabusu kwa muda mrefu bila kuwafikisha mahakamani.
Hata hivyo, alisema wakiwa nje kwa dhamana, jeshi lake litaendelea na upelelezi na kuwahoji kila litakapokuwa likihitaji kufanya hivyo.
“Tumeamua kuwaachia sababu sheria haituruhusu kuendelea kuwashikilia muda mrefu na lengo letu hasa katika hili tukio hatutaki kumwonea mtu yeyote, ndiyo sababu tunafanya uchunguzi wa kina,” alisema.
Alisema hadi sasa hakuna ongezeko la mtu mwingine aliyefikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo zaidi ya Victor Ambrose Kalist (20).
Victor alifikishwa mahakamani Mei 13 mwaka huu, mbele ya Kaimu Hakimu Mwandamizi Mkazi wa Arusha, Devotha Kamuzora, kujibu mashtaka mawili ya kuua na kujaribu kuua na kesi yake itatajwa tena Mei 27, mwaka huu.
Watuhumiwa walioachiwa kwa dhamana ni Jassin Mbarak (29) mkazi wa Bondeni Arusha, Joseph Lomayani (18)
dereva wa pikipiki na mkazi wa Kwa Mrombo Arusha, George Batholomeo Silayo (23) mfanyabishara mkazi wa Olasiti na Mohamed Suleiman Said (38) mkazi wa Ilala Dar es Salaam.
Mei 13 mwaka huu, Kamanda Sabas, alisema watuhumiwa watatu raia wa UAE ambao ni Abdul Aziz Mubarak (30) mfanyakazi Mamlaka ya Mapato, Fouad Saleem Ahmed al Hareez al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha Zimamoto na Saeed Abdulla Saad (28) ambaye ni askari polisi wa kitengo cha usalama barabarani, pamoja na raia wa Saudi Arabia, Al-Mahri Saeed Mohseens (29) waliachiwa huru baada ya kubainika kuwa hawakuwakupatikana na kosa la kuwafungulia mashitaka.
Tukio la kurushwa kwa bomu hilo lilisababisha mauaji ya watu watatu na wengine zaidi ya 67 kujeruhiwa.

Subscribe to:
Posts (Atom)